MICHEZO

Ibrahim Ajibu Awaomba Radhi Mashabiki Wa Yanga Kwa Kukosa Penalt

on

Baada ya kupata kipigo cha penalti 5-4 dhidi ya URA, juzi mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu Migomba ameom­ba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo kuto­kana na ma­tokeo ma­baya.

Yanga ilion­dolewa kwenye michuano ya Kombe la Map­induzi katika hatua ya nusu fainali na URA ya Uganda kutinga fainali dhidi ya Azam FC.

Msham­buliaji huyo alisema hawakupenda kupata matokeo ya aina ile lakini ilitokea vile kwa sababu mpira una matokeo matatu.

“Naomba mashabiki wetu wa Yanga wa­tusamehe kwa matokeo mabaya hakuna timu ambayo inapenda kupoteza zaidi mtupe sapoti ,”al­isema Ajibu.

Hata hivyo katika mchezo huo wachezaji ambao wali­piga penalti ni Papy Tshishim­bi, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Daud Raphael na Obrey Chirwa ambaye alikosa.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login