ELIMU

Hakuna Michango Yoyote Katika Shule Aagiza Rais Magufuli

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kukazia sera yake ya elimu bure ambapo awamu hii amepiga marufuku michango yote inayochangishwa mashuleni.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatano Januari 17, 2018 Ikulu, jijini Dar es salaam alipokutana na Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.Hata hivyo, Rais Magufuli amewataka Mawaziri hao kusimamia agizo hilo kwa shule zote za Sekondari na Msingi ili kuondoa adha ya michango.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login