Chadema Wapata Jeraha Tena...Madiwani Watatu Wahamia CCM - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

SIASA

Chadema Wapata Jeraha Tena…Madiwani Watatu Wahamia CCM

on

Wakati chama cha mapinduzi CCM kikiendelea kujipatia wafuasi kutoka upinzani sasa, Imeelezwa kuwa Madiwani watatu wa CHADEMA katika halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha, wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ( CCM).

Madiwani hao ni Jacob Silas Mollel wa Kata ya Elang’atadapash, Elias Mepukori Mbao wa Kata ya Kamwaga na Diyoo Lomayani Laizer Kata ya Olmolog.

Sababu za kujiunga CCM ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi, kuinua uchumi na pia kurejesha nidhamu kazini.

Tukio hilo limejiri ikiwa ni siku moja tu imepita tangu aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CHADEMA Taifa, Muslim Hassanali atangaze kukihama chama hicho na kujiunga CCM.

Mfululizo wa Madiwani wa CHADEMA kuhamia CCM umekuwa mkubwa mwaka huu kwani kwa mwezi Januari pekee hadi sasa ni Madiwani watano waliokihama chama hicho.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login