MICHEZO

Azam Yawapania URA Kombe La Mapinduzi Katika Fainali

on

Kikosi cha timu ya Azam FC.

Nahodha wa Azam FC, Himid Mao amefunguka kuwa anaamini watapata ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya URA, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Akizungumza na Championi Iju­maa, Mao alisema hadi kufikia fain­ali wamepambana na ni kitu kizuri lakini akasema safari hii wataongeza nguvu ili wakamilishe kazi kwa kut­waa ubingwa wa michuano hiyo.

Timu ya URA. 

Amesema kuwa wapinzani wao wana timu nzuri lakini watapam­bana nao, kauli ambayo iliungwa na mshambuliaji wa Azam FC, Shabani Iddi wa Azam FC ambaye alisema mbali na kujituma atatumia mchezo huo kuonyesha kuwa yupo fiti kwa ajili ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

“Umeona nimerejea uwanjani la­kini bado sijawa fiti kwa silimia zote, nashukuru kwa kupewa nafasi la­kini tutapambana ili kuwa mabing­wa,” alisema Idd.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login