Azam FC Yatwaa Ubinngwa Kombe La Mapinduzi Huko Zanzibar - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MICHEZO

Azam FC Yatwaa Ubinngwa Kombe La Mapinduzi Huko Zanzibar

on

Klabu ya Azam FC jana usiku imefanikiwa kutetea kombe la Mapinduzi kwa kuifunga klabu ya URA kutoka Uganda kwa goli 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 za kawaida.

Ushindi huo wa jana wa Azam FC unakuwa ni ushindi wa nne tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 2007 ambapo imetwaa kombe hilo mwaka 2012, 2013, 2017 na 2018.

Klabu ya Azam FC kwa sasa inakuwa ndiyo klabu iliyochukua makombe mengi zaidi ikifuatiwa na Simba SC ambayo imechukua mara tatu huku klabu za Yanga SC, Miembeni FC, Mtibwa Sugar na KCCA zikitwaa kombe hilo mara moja.

Kwa rekodi nyingine ni kwamba Azam FC ndio klabu pekee iliyoweza kutetea ubingwa wake kwenye michuano hiyo awali hakukuwa na klabu iliyowahi kufanya hivyo.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login