SIASA

FAHAMU:Hawa Ndio Viongozi Wanne Afrika Waliojiapisha Kama Raila Odinga

on

Hapo jana, January30, 2017 kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga alijiapishwa kuwa ‘rais wa wananchi’ nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika mwaka jana.

Hata hivyo Raila Odinga si kiongozi wa kwanza kitu kama hicho barani Afrika, kuna hawa wengine wanne.

1.         Kizza Besigye

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, kupitia kanda ya video alionekana akifanya sherehe za kula kiapo kuwa Rais wa Uganda baada yake kushindwa uchaguzini mwaka 2016 na Bw Museveni.Kufuatia tukio hilo, Besigye amekuwa akikamatwa na kushtakiwa mara kwa mara nchini humo.

2.          Etienne Tshisekedi

Etienne Tshisekedi alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Sese Seko Zaire, na baadaye Laurent Kabila Joseph Kabila wa DRC

November 2011 Tshisekedi aliposhindwa katika uchaguzi dhidi ya mtoto wa Laurent Kabila, aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha katika uwanja wa Wahanga, Kinshasa kutibuka.

3.         Moshood Abiola

Baada ya kutembelea nchi nyingi za Magharibi kutafuta msaada ili kumkabili aliyekuwa Rais wa Nigeria, Sani Abacha katika utawala wake, Moshood Abiola alijitangaza mwenyewe kuwa rais wakati Rais Abacha bado yupo madarakani.

Hata hivyo baadaye Abiola alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela kwa miaka minne hadi mwaka 1995.

4.          Jean Ping

Jean Ping kiongozi wa upinzani Gabon mwaka 2016 alijitangaza mwenyewe kuwa rais na kutoa wito kura kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Ali Bongo ameshinda. Hata hivyo dunia nzima alijua kwamba Ping ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo.

ADD YOUR COMMENTS