BURUDANI

Nandy Amuanika Rubby Katika Media

on

Msanii wa muziki Bongo, Nandy amejibu kauli ya Ruby ambayo ilidai alikaa kimya kimuziki kumpisha muimbaji huyo kufanya vizuri.

Nandy amesema hilo halina ukweli wowote kwani tangu alipoondoka katika uongozi wake kuna nyimbo ambazo alitoa, hivyo kutoa kauli kama hiyo ni kujitetea.

“Sio kweli kwa sababu nakumbuka ana nyimbo tatu kazitoa kipindi ambacho amesema amepumzika, katoa singeli mbili na wimbo mmoja unaitwa Wale Wale, sasa hapo alikuwa amepumzika au ni kitu ambacho si cha kweli,Halafu watu walikuwa wanajua amegombana na uongozi wake ndio akatoa hizo nyimbo ni kisingizio cha kujitetea,” Alisema Nandy.

Kwa sasa Nandy anafanya vizuri na wimbo ‘Subal kheir’ alioshirikiana na Aslay ambao awali uliimbwa na Culture Group kutoka visiwani Zanzibar.

ADD YOUR COMMENTS