BURUDANI

Huenda Jay Z Asipige Show Tuzo Za Grammy Mwaka Huu

on

Je ulikuwa unatamani kuiona show ya Jay Z kwenye tuzo za Grammy mwaka huu? Basi msanii huyo kunauwezekano asifanye hivyo katika utoaji wa tuzo hizo ambapo utafanyika Jumapili ya January 28 katika viwanja vya Madison Square Garden jijini New York nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao wa HITS Daily Double, umesema Jay amejitoa katika orodha ya wasanii ambao watafanya show hiyo kwa sababu zisizojulikana.

Mwaka jana rapper huyo hakufanya show hiyo lakini alikuwa jukwaani akimtazama mkewe Beyonce ambaye alitumbuiza kwa mara yake ya kwanza mbele ya umma baada ya kuwa mjamzito wa mapacha wao Rumi na Sir ambao walizaliwa mwezi Juni mwaka jana.

Wasanii wengine ambao walitajwa kutumbuiza katiKendrick Lamar, Rihanna, Bryson Tiller, DJ Khaled, Bruno Mars, Cardi B, SZA, Childish Gambino, Logic, Alessia Cara, Khalid, Lady Gaga, U2, Miley Cyrus na Elton John.

Wakati huo huo Jay Z ameongoza kwa kutajwa kwenye vipengele vingi zaidi vya wasanii wanaowania tuzo hizo, ambapo ametajwa katika vipengele 8.

ADD YOUR COMMENTS