BURUDANI

Mkali Wa Muziki Wa Zamani TID Mnyama Awaanika Wanii Wa Sasa

on

Msanii wa muziki, TID amedai nyimbo za wasanii wa zamani zilikuwa zinadumu muda mrefu zaidi kutokana na wasanii hao kutumia muda mwingi zaidi kuandaa nyimbi zao.

Muimbaji huyo amedai nyingi za siku hizi zinashindwa kufanya vizuri na kudumu kutokana na kuandikwa kiwepesi wepesi.

“Nyimbo nyingi za zamani tulikua tunatumia muda kuandika pia hata waandaji wanafanya ‘mixing’ vizuri tofauti na ngoma za siku hizi zina copy kutoka nje ndio maana hazidumu”alizungumza  TID.

TID amesema wasanii wanatakiwa kuacha kucopy nyimbo za nje ili muziki wa Tanzania uendelee kukuwa.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login