MAGAZETI

Meli Urusi Yadaiwa Kupeleka Mafuta Korea Kaskazini

on

Maafisa wawili wa usalama barani Ulaya wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba malori mawili ya mafuta kutoka Urusi yaliwasilisha mafuta huko Korea Kazkazini hivyo kukiuka azimio la umoja wa mataifa la kuzidisha vikwazo zaidi dhidi ya utawala huo wa Pyongyang ili kujaribu kukomesha mradi wake wa kutengeneza silaha za kinuklia.

Wanasema malori hayo yaliyosafirishwa kwa meli yalionekana katika picha za Satellite zilizo karibu na bandari za Urusi upande wa pwani ya Pacific na kuthibitishwa kwa duru za kiintellijensia .

Hata hivyo mmoja wa maafisa hao ameongeza kusema kuwa bado hamna ushahidi wowote kwamba serkali ya Urusi imehusika na usafirishwaji wa shehena hiyo.

Meli husika ambayo iko chini ya leseni ya Hong Kong ilikamatwa na maafisa wa Korea Kusini lakini mwenye meli hiyo amekana kuhusika na swala hilo.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login