MICHEZO

Manchester CityYatinga Nusu Fainali Kombe La EFL

on

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la EFL baada ya kuichakaza Leicester City goli 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Manchester City na Leicester City wamefikia hatua ya penati baada ya kutoka goli 1-1 ndani ya dakika 120 ya mchezo huo wa robo fainali ya kombe la EFL.

Goli kipa wa Manchester City, Claudio Bravo ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo baada ya kucheza penati ya mshambuliaji wa Leicester City, Riyad Mahrez huku Jamie Vardy akikosa penati kwa kupiga nje ya goli.

Klabu nyingine iliyofuzu nusu fainali ya kombe la EFL ni Arsenal kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya West Ham United.

Leo kutachezwa mchezo mwingine wa robo fainali ya pili, ambapo Klabu ya Manchester United itavaana na Bristol City huku wazee wa darajani Chelsea watawakaribisha AFC Bournemouth.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login