Esther Akoth ‘Akothee’ Atamani Kuzaa Na Meneja Wake Mapacha - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

BURUDANI

Esther Akoth ‘Akothee’ Atamani Kuzaa Na Meneja Wake Mapacha

on

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Esther Akoth ‘Akothee’ ameonesha kutamani  watoto mapacha kwa meneja wake ‘Nelly Oaks’ ambaye amekuwa akimkana kila alipoulizwa kama wanatoka kimapenzi naye.

Kupitia ukurasa wa Instagram msanii huyo Akothee, aliweka ujumbe ulioelezea shauhuku yaKe ya kupata watoto watatu mapacha kwa mara moja na meneja wake Nelly ili kuondoa maneno maneno ya baadhi ya waosema sana kuhusu wao kupata watoto.

“Baby , I just want to have triplets for you , so they can abuse us in one pregnancy iishe 😂😂😂if we start dropping one after another some will give up on the way due to lack of new insults😂😂 and you know we don’t need common insults we need new ones for every episode @nellyoaks#callpolis”.

Hata hivyo Akothee alishakana mara kadhaa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi licha ya picha kueleza huba wa wazi wazi uliopo kati yao kiasi mtoto wa kike wa Akothee ‘Celly Rue Brown’ kuingia katika moja ya picha aliyopost Nelly akiwa na Akothee na kuandika maoni yake kuwa wawili hao wamezidisha kuonesha kuwa wanapendana.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login