BURUDANI

Siri Wazi Sasa Akothee a.k.a Madam Boss Ajiachia Na Bosi Wake Nelly Oaks

on

Msanii wa muziki na mjasiriamali kutoka nchini Kenya Akothee a.k.a Madam Boss, amewagusa nakuwakosha nyoyo za mashabiki wake pale alipotupia picha zenye muonekano wakuwa yupo kwenye mahaba na meneja wake wa muziki Nelly Oaks. Nelly Oaks ambaye pia anamakazi yake nchini Canada, wengi wanamfahamu kama maneja anayesimamia kazi za muziki za staa wa muziki na tajiri huyu wa nchini Kenya Akothee.

Akothee ambaye pia ni mama wa watoto watano, amekuwa haoni haya kuweka wazi bayana kuwa watoto hao wote kila mmoja anababake mzazi. Kwasasa staa huyo ambaye yupo ughaibuni ambako anatarajiwa kufanya tour kwenye mataifa matatu tofauti ya Ulaya ikiwemo Canada, Ujerumani na USA. Lakini kupitia tour hii ndipo ameamua kuweka wazi kuwa yeye na meneja wake nikama kitu kimoja kwasasa, awali Akothee alishawahi kunukuliwa akisema kuwa haogopi kuzaa na yuko tayari wakatiwowote kuzaa bora apate mwanamume anayemfaa.

Mwakajana Akothee alipata pigo la kupoteza ujauzito, ambapo alitarajiwa kujifungua mapacha ila kwabahati baya ujauzito ule ukaavya. Hata hivyo baada ya kupata pigo hilo, aliachana uhusiano wake na mwanamume huyo aliyemumpa ujauzito huo ambaye alikuwa na asili ya kizungu. Hata hivyo baada ya kukata uhusiano na mzungu huyo Akothee ameonekana kuwa single nakwamda sasa hajaonekana kuwa karibu na mwanamume mwingine ila maneja wake Nelly Oaks.

Hata hivyo licha ya tetesi za chini kwa chini kuhusu uhusiano wake na meneja wake, Akothee ameonekana kutojali maneno yasemwayo juu ya uhusiano wake na ndiomaana akaamua kufunguka wazi kwa picha hizi zinazoonyesha kuwa yupo kwenye mahaba mazito ama wasemavyo walumbi kuwa ni mapenzi mbashara baina ya Akothee na Meneja wake.

ADD YOUR COMMENTS

Recommended for you