MUZIKI

Nyimbo mpya ya Ommy Dimpoz haikamatiki YouTube

on

Angalau kwa sasa Ommy Dipoz anaweza akapumzika baada ya kuutua mzigo mzito wa lawama kutoka kwa mashabiki wake kuhusu kuchelewa kutoka kwa video ya wimbo wake mpya ‘Cheche’.

Hata hivyo hali hiyo inaweza ikawa ni neema kwa msanii huyo kutokana na mashabiki kutamani kuiona kwa muda mrefu. Video hiyo kufanikiwa kushika namba moja kwenye trending ya mtandao wa YouTube na kuzipiga chini video nyingine zilizouteka mtandao huo ikiwemo ‘Seduce Me’ ya Alikiba, ‘Zilipendwa’ ya WCB na ‘Unaibiwa’ ya Rayvanny.

ADD YOUR COMMENTS