MAZINGIRA

Liberia Watoa Msaada Kwa Sierra Leone Kutokana na Janga La Maporomoko Ya Ardhi

on

Timu ya kusaidia katika hali za dharura kutoka Liberia imewasili nchini Sierra Leone siku ya Alhamisi kuisaidia kujipanga upya baada ya maporomoko ya udongo kutokea katika mji mkuu na kusababisha vifo vya watu takriban 400.

Kwa mujibu wa habari,timu hiyo inahusisha wanajeshi kutoka Liberia,timu ya msalaba mwekundu na mashirika ya kiserikali ambapo kwa ujumla wataisaidia Sierra Leone kusambaza huduma ya afya kwa waathirika.

Rais wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf aliyewasili nchini Sierra Leone kabla ya timu hiyo kufika anatarajia kukutana na rais Ernest Bai Kromah kuonyesha mshikamano kwa serikali na wananchi kwa ujumla hasa baada ya janga hilo kutokea.

Rais wa Liberia amesema jinsi nchi yake ilivyosikitishwa na kutokea kwa maporomoko hayo nchini Sierra Leone na kuahidi kuwa nao bega kwa bega mpaka mwisho.

Mamia ya watu walipoteza maisha na wengine wengi kunaswa ndani ya majumba yao baada ya maporomoko ya udongo kutokea katika mji mku wa Freetown baada ya mvua kali kutokea nchini Sierra Leone siku ya Jumatatu.Ripoti zinaonyesha kuwa takriban watu 600 bado hawajulikani walipo.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login