Waziri Wa Usalama Nnchini Kenya Joseph Nkaissery Afariki Dunia Asubuhi Hii - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

HADITHI

Waziri Wa Usalama Nnchini Kenya Joseph Nkaissery Afariki Dunia Asubuhi Hii

on

Waziri wa usalama nchini Kenya Jenerali Joseph Nkaissery amefariki dunia.

Habari kutoka Ikulu ya Nairobi imesema kuwa, Wazir Nkaissery alifariki dunia saa chache baada ya kulazwa ghafla katika hospitali ya Karen jijini Nairobi. Kifo cha Nkaissery kimewashtua wakenya waliomkia habari hii  mbaya siku hii ya Jumamosi.

Mara ya mwisho kuonekana hadharini ilikuwa siku ya Ijumaa wakati wa maombi ya wagombea urais katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi na kuonekana kuwa mwenye afya.

Kifo hiki kimetokea siku 30 kamili kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini humo. Nkaissery aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama mwaka 2014 akitokea chama cha upinzani cha ODM. Kati ya mwaka 2008-2013 alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi katika serikali ya muungano. Alikuwa mbunge wa zamani wa upinzani jimbo la Kajiado ya Kati kwa miaka 12.

Haijafahamika kilichosababisha kifo chake.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login