Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #5 - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

HADITHI

Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #5

on

Sehemu ya5

Ikauli kwa kumtajia jina langu.
“Haya Prince, kwa hiyo chakula gani?”.Aliniuliza.
“Kalete kile unachoona kitanifaa mimi”.Nikamjibu huku namuangalia usoni.Hadi hapo nilikuwa namjibu majibu yangu kisomi zaidi. Kama angeelewa nachomaanisha,sidhani kama angeuliza swali linalo fuata.
“Ok! Na kinywaji gani?”.
“Hicho niletee chako mwenyewe”.Nikamjibu.
“Changu mwenyewe kivipi?”.Akazidi kunichimba maswali.
“Kwani wewe una kinywaji gani?”.
“Mimi sina kinywaji”.
“Okey! Nitakwambia baadaye. Sasa hivi niletee chochote utakachokiona”.Nikamjibu na baada ya jibu hilo,akatoka kwa ajili ya kwenda kufanya nilichomuagiza.
Huku nyuma mimi nikabaki nawaza na kuwazua jinsi ya kumuingia yule Nesi Subira ambaye ndiyo alifanya hata ile sehemu ya kati ya shuka la hospitali ile kuwa kama pana panda na kushuka.Baada ya kuwaza sana, niliamua saa nne au saa tano za usiku ule ndiyo nifanye niliyotumwa na shetani.Baada ya dakika kama kumi na tano,Nesi Subira aliingia na kimfuko cheusi kidogo kilichosheheni chips mayai ndani yake pamoja kuku nusu. Wakati huo mkono wake wa kushoto alikuwa kabebelea maji ya kunywa na soda aina ya fanta.
“Dah! We dada unajua sana. Hivi ulijuaje kuwa napenda fanta?”.Nikamuuliza swali lingine la kisomi huku nikimaanisha fanta ni yeye kutokana na rangi aliyokuwa nayo.

ADD YOUR COMMENTS

401 Comments

  1. kobe bryant shoes

    September 21, 2017 at 5:49 am

    This post is actually a pleasant one it assists new internet people, who are wishing for blogging.
    kobe bryant shoes http://www.kobebryantshoes.us

You must be logged in to post a comment Login