BannerFans.com

MICHEZO

MANCHESTER UNITED KUMKOSA RUSHFORD KATIKA MICHEZO KADHAA

on

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford atatajwa kwenye kikosi cha meneja wa England , Gareth Southgate siku ya Alhamisi.Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 hapo awali alitarajiwa kushirikishwa katika upande wa vijana mwenye chini ya umri wa miaka 21 watapokuwa wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani na Denmark wikendi ijayo. 
Lakini na washambuliaji wa England Harry Kane na Wayne Rooney wote wametolewa kutokana na majeraha , huko Rashford akitarajiwa kuchukua nafasi hiyo.England itakabiliana na Ujerumani katika mechi ya kirafiki kabla ya mchuano wa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania huko Wembley tarehe 26 mwezi Machi .
Chelsea yaizaba Man Utd 1-0 Kombe la FA
Rashford alifunga goli katika mechi yake ya kwanza na England walipopata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Australia mwezi Mei mwaka Jana na wamejizolea vikombe sita vikuu.Manchester United ilimchezesha katika dakika za mwisho waliposhindwa kwa bao 1-0 dhidi ya Chelsea katika kombe la FA siku ya Jumatatu , licha ya kutolewa katika kikosi cha hapo awali kutokana na maradhi.
Man United kukabili Chelsea bila Rooney
Nahodha wa England , Rooney aliwachwa nje ya safari ya Manchester United ya kuelekea katika mji kuu kutokana na jeraha alilolipata alipogongana na mwenzake walipokuwa wakifanya mazoezi.Na mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane pia alitolewa nje ya uwanja kutokana na jeraha la kifundo cha mguu walipokuwa wakiminyana na Millwall siku ya Jumapili.Klabu ya Spurs imesema jeraha hilo linafanana na lile alilolipata mwezi Septemba wakikabiliana na Sunderland .

ADD YOUR COMMENTS

271 Comments

  1. Pingback: true religion store online

You must be logged in to post a comment Login